Klabu ya Tottenham Hot Spurs imepoteza mechi yake ya kwanza hii leo kwenye ligi Kuu ya Uingereza baada ya kupokea kipigo kikali cha mabao 3-1 kutoka kwa Arsenal kwenye Dabi ya London ambayo imepigwa majira ya saa 14:30.

 

Spurs Yapoteza Mechi Yake ya Kwanza.

Spurs kufikia leo hii alikuwa hajapoteza mchezo wowote baada ya kucheza michezo yake saba, na hatimaye amekuja kupoteza hii leo, ambapo baada ya kupata adhabu ya kadi nyekundu kwa Emerson. Spurs alielemewa na kuwaruhusu The Gunners waongeze bao la tatu na mchezo kumalizika hivyo hivyo.

Hivyo basi mpaka sasa Antonio Conte na timu yake wanashikilia nafasi ya 3 kwenye msimamo baada ya michezo 8 ambayo ameshacheza, huku anayemfuata akiwa na alama 13 na michezo miwili mkononi ambaye ni Brighton.

 

Spurs Yapoteza Mechi Yake ya Kwanza.

Dabi ya London imemalizika kwa Arteta akitoka kifua mbele nyumbani kwake kwa ushindi mnono ambao unawafanya wazidi kuimarika huku wakilitaka taji la ligoi kuu kama wakiongeza juhudi.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa