Harry Kane mshambuliaji wa klabu ya Tottenham na timu ya taifa ya Uingereza amefanikiwa kua mchezaji wa kwanza kufunga magoli 100 ugenini katika ligi kuu ya Uingereza.
Harry Kane amefanikiwa kuweka rekodi hiyo baada ya kufunga katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza mapema leo dhidi ya mahasimu zao klabu ya Arsenal ambapo katika mchezo mshambuliaji huyo alifunga bao moja na kumfanya aweke rekodi hiyo licha ya klabu yake kupoteza mchezo huo kwa magoli matatu kwa moja.
Harry amefanikiwa pia kuweka rekodi nyingine baada ya kufunga katika mchezo huo na kua mfungaji wa muda wote wa dabi za jiji la London baada ya kumpiku gwiji wa klabu ya Arsenal Thiery Henry ambae amekua akiongoza kwa muda mrefu akifuatiwa na Frank Lampard lakini mshambuliaji huyo amevunja rekodi hiyo baada ya kufunga leo.
Harry Kane amekua mshambuliaji mwenye ubora na kuendeleza ubora kwa misimu kadhaa na kufanikiwa kua mfungaji bora kwenye ligi hiyo mara kadhaa na wengi wkimtabiria kuvunja rekodi ya gwiji wa zamani wa ligi hiyo mfungaji bora wa muda wote wa ligi hiyo Alan Shearer.