Kocha mkuu wa Juventus Massimiliano Allegri ametangaza msimu wao  mpya unaanza dhidi ya Bologna kufuatia kuanza vibaya kwenye Serie A msimu huu.

 

Allegri Atangaza Msimu Mpya.

Vijana wa Allegri hawajashinda katika mechi tano, huku wakiwa wamepoteza mechi mfululizo ikiwemo ile ya mwisho waliyopoteza dhidi ya Monza kwenye Serie A na Benfica kwenye Ligi ya Mabingwa kabla ya mapumziko ya Kimataifa.

Presha inazidi kuongezeka kwa kocha huyo kutokana na matokeo hayo ambayo hayaridhishi huku Juventus wakiwa wameshinda mechi mbili pekee kati ya tisa msimu huu. Allegri alisema;

“Tulikuwa tumeanza vyema katika mechi tatu za kwanza, kisha kulikuwa na kushindwa mara nyingi na matokeo mabaya. Kuanzia kesho msimu mpya lazima uanze,” alisema katika mkutano na waandishi wa habari Jumamosi”.

Allegri Atangaza Msimu Mpya.

Juventus inaweza kurudi kwenye ubora wake endapo wachezaji kadhaa watarejea ambao ni  Adrien Rabiot, Manuel Locatelli na Alex Sandro wakiwa miongoni mwa waliorejea kwenye kikosi, huku Allegri akipangwa kusimamia timu hiyo katika kipindi hicho kigumu.

“Lazima nisimamie wachezaji muhimu kwa njia bora zaidi kwasababu sasa tutakuwa na mechi nyingi za karibu,” aliongeza.

Alisema kuwa wanarejesha wachezaji muhimu Tunawarejesha, Sandro, Rabiot na Locatelli, Juan Cuadrado na Arkadiusz Milik wanarejea kutoka kwa kutofuzu. Ni Angel Di Maria pekee aliyesalia nje, kutokana na kufungiwa, Paul Pogba na Federico Chiesa.”

 

Allegri Atangaza Msimu Mpya.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa