Golikipa wa Chelsea Kepa Arrizibalaga ameapa kuchukua nafasi ya “mwanzo mpya” katika klabu hiyo baada ya kuteuliwa kwa Graham Potter msimu huu baada ya kuondoka kwa Thomas Tuchel.
Kipa huyo wa Hispania aliondolewa kama chaguo la kwanza la Chelsea na Eduard Mendy wakati mchezaji huyo wa Taifa la Senegal alijiunga kutoka Rennes September 2020, na amekuwa katika kikosi cha kwanza cha Chelsea tangu wakati huo.
Kepa alicheza mechi 15 pekee msimu uliopita, Ikijumuisha mechi mbili kama mchezaji wa akiba, Lakini aliweka asilimia 80.8 ya kuokoa, huku Mendy akisimamia asilimia 70.8 pekee katika michezo yake 49.
Mendy alianza msimu huu kama chaguo la kwanza la Tuchel, Lakini kufukuzwa kwa kocha huyo wa Kijerumani kunaweza kuwa na uteuzi mpya katika kikosi hicho ambacho kunamaanisha kuwa na mpangilio safi.
Sasa Kepa anatumai kuwa kunaweza kuwa na nafasi ya yeye kujitangaza kuwania kushika jezi hiyo, baada ya kucheza mechi mfululizo za ligi ya mabingwa baada ya majeraha ya Mendy.
“Msimu uliopita nilipocheza nilijisikia vizuri sana, Lakini ilikuwa ni mechi 15 tuu au kitu kama hiki” Kepa alisema akinukuliwa kwenye tovuti ya Chelsea. “Sio kiasi kikubwa, hivyo sasa ninapopata nafasi najaribu kufanya niwezavyo na kuisaidia timu kama nilivyofanya kwenye michezo iliyopita
Aliendelea kwa kusema kuwa anafurahishwa na uchezaji wake, na anafurahishwa kucheza ligi za Mabingwa uwanjani hivyo ni mwanzo mpya, na nina furaha na ninaukubali. Chelsea wameanza kampeni zao za Ulaya kwa kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Dinamo Zagreb, na kufuatiwa na sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya Salzburg katika mchezo wa kwanza wa Potter, Hivyo matokeo yanaweza kuwa bora zaidi.
Ujio wa Potter kutoka Brighton umekuja wakati kampeni ya ligi kuu ya Chelsea imesitishwa na mechi dhidi ya Fulham na Liverpool kuahirishwa kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth.