Laporte Anukia Al-Nassr

Beki wa klabu ya Manchester City raia wa kimataifa wa Hispania Aymeric Laporte inaelezwa yuko mbioni kutimkia Saudia Arabia kujiunga na klabu ya Al-Nassr ya nchini humo.

Beki Laporte ambaye alikua anafukuziwa na klabu ya Arsenal lakini klabu ya Manchester City imekubali ofa kutoka klabu ya Al Nassr, Hivo kilichobaki ni mchezaji huyo kukubaliana na klabu hiyo ili kujiunga nao.laporteKlabu ya Al-Nassr imeeleza kuweka ofa nzuri kwa klabu ya Manchester City ambao wameonesha taa ya kijani kwa Al Nassr, Hivo ni suala la klabu hiyo kukaa chini na beki huyo ili kumalizana nae kwenye maslahi binafsi ili kumsajili mchezaji huyo.

Beki huyo raia wa kimataifa wa Hispania mpaka sasa imeonekana hayupo kwenye mipango ya klabu ya Manchester City chini ya kocha Pep Guardiola, Hivo ni yeye sasa anatakiwa kuamua kukubaliana na klabu hiyo kutoka Saudia ili aweze kujiunga nao.laporteBeki Aymeric Laporte amekua na kiwango bora ndani ya klabu ya Manchester City tangu amejiunga na timu hiyo akitokea klabu ya Sevilla, Lakini inaonekana muda wa kutimka ndani ya timu hiyo na kujiunga na klabu ya Al-Nassr

Acha ujumbe