Mshambuliaji wa Barcelona Robert Lewandowski ameipaisha timu yake hadi kileleni kwa Laliga baada ya kufunga bao katika dakika za lala salama za 90+3 huku akipewa pasi ya bao kutoka kwa Raphina.

 

Lewandowski Aipaisha Barcelona Kileleni.

Bao hilo la Lewandowski limewafanya wafikishe pointi 31 wakiwa sawa na Real Madrid ambapo tofauti yao ikiwa ni magoli ya kufunga na kufungwa huku Madrid wakiwa na mchezo mmoja mkononi ambao watacheza leo dhidi a Girona.

Kocha mkuu wa Valencia Gennaro Gattuso amesikitika kwa kutochukua kitu baada ya kucheza vizuri hapo jana na kuja kuruhusu bao katika dakika za lala salama.

Lewandowski Aipaisha Barcelona Kileleni.

Lewandowski na timu yake wiki hii watacheza dhidi ya Viktoria Plizen kwenye mchezo wa Klabu Bingwa ambao ni wakukamilisha ratiba yake baada ya kuondolewa kwenye michuano hiyo hivy kwenda Europa.

Katika kundi hilo ni Viktoria Plizen peke yake ambaye kapoteza michezo yote hivyo imekuwa ni rahisi sana kwa Barca kwenda michuano ya Europa tofauti na makundi mengine ambayo timu inabidi ishinde mchezo wa mwisho ili iweze kufuzu Europa.

Lewandowski Aipaisha Barcelona Kileleni.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa