Lewandowski Atwaa Tuzo ya Mshambuliaji Bora Duniani.

Robert Lewandowski ameshinda Kombe la Gerd Muller kwa kufunga mabao 57 kwa klabu na nchi msimu uliopita na hayuko tayari kukwepa changamoto ya kuandamwa na Erling Haaland katika kampeni ya 2022-23.

 

Lewandowski Atwaa Tuzo ya Mshambuliaji Bora Duniani.

Lewandowski alitunukiwa tuzo hapo jana kwenye usiku wa Ballon d’OR amechukua tuzo hiyo kama mshambuliaji bora wa Dunia kwa mwaka wa pili mfululizo kabla ya Karim Benzema kutwaa tuzo ya Ballon d’Or kwa mara ya kwanza.

Heshima hiyo ya mshambuliaji Bora wa Mwaka imepewa jina la Muller, mshambuliaji  mashuhuri wa Bayern Munich ambaye Lewandowski alivunja rekodi yake ya mabao 40 msimu mmoja katika Bundesliga akiwa njiani kutwaa taji hilo.

Lewandowski Atwaa Tuzo ya Mshambuliaji Bora Duniani.

Lakini ikiwa mchezaji huyo wa Barcelona atahifadhi tuzo hiyo kwa mara nyingine tena mwaka wa 2023, itamlazimu kumshinda mfungaji bora wa Manchester City, Haaland. Mchezaji huyo nambari tisa wa City ana mabao 20 kwa klabu tayari, pia ameifungia Norway mara moja msimu huu.

Wakati huohuo, Lewandowski, ambaye alikuwa mchezaji wa nne bora katika viwango vya Ballon d’Or, ana mabao 14 kwa Barcelona mpaka sasa.  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 aliulizwa kuhusu Haaland alipokuwa akipokea Tuzo ya Muller kwenye sherehe ya Ballon d’Or, huku Didier Drogba akimwambia kuhusu mshambuliaji wa Haaland ambaye amewaka moto msimu huu.

Lewandowski Atwaa Tuzo ya Mshambuliaji Bora Duniani.

Lewandowski alisema: “Msimu ni mrefu sana, na najua kwangu pia ni ukurasa mpya na Barcelona. Tangu siku za kwanza, ninahisi vizuri sana katika klabu hii.

Kuanzia dakika za kwanza naona nikiwa na wachezaji wenzangu tuna uwezo mkubwa na nina nafasi ya kufunga mabao mengi, nina uhakika wote kwa pamoja tunalifanyia kazi hili. Aliongeza kwa kusema kuwa hili ni soka na wanapaswa kuwa tayari kila wakati na kizazi kipya kinakuja lakini bado yupo hapo.

Lewandowski ana furaha sana na anajivunia sio tu kushinda lakini pia kwasababu ya jina la kombe hilo huku akisema kuwa Gerd alikuwa na msukumo mkubwa akisisitiza kuwa kabla ya msimu alitaka kuwa karibu naye na siku zote alikuwa akitaka kuvunja baadhi ya rekodi zake na ilikuwa changamoto kubwa kila mara.

Roberto amesema kuwa ilikuwa ni hisia sana kufunga mabao 41 katika Bundesliga kwasababu hakufikria kama ingewezekana kuvunja rekodi hiyo na kila alichofanya ni kwaajili yake.

Wakati ofa ya Haaland ikisubiri mwaka mwingine, kwani alifunga mara 42 kwa Borussia Dortmund na Norway kwa pamoja, City hawakuondoka mikono mitupu.

Lewandowski Atwaa Tuzo ya Mshambuliaji Bora Duniani.

Mabingwa hao wa watetezi wa Ligi kuu ya Uingereza ya  wamewashinda washindi wa fainali ya Ligi ya Mabingwa, Liverpool na Real Madrid na kuwania tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka.

Acha ujumbe