Robert Lewandowski Ashinda Tuzo yaMshambuliaji Bora wa Dunia

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Robert Lewandowski ameshinda tuzo ya Muller na kutambulika kama mshambuliaji bora duniani kwenye msimu wa  2021/22.

Robert Lewandowski ameshinda tuzo huyo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kushinda tuzo hiyo msimu uliopita na kuipa jina la mshumbuliaji wa Ujerumani ambaye aliaga dunia agosti 2021, ambapo awali ilitambulika kama mshambuluaji bora wa mwaka.

Robert Lewandowski msimu wa 2021/22 alifanikiwa kuweka kimyani goli 50 kwenye michezo 46 kwenye mashindano yote aliyocheza akiwa na Bayern Munich na kufanikiwa kuchukua liatu cha dhahabu mara mbili mfululizo na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee kutoka nje ya Ujerumani kufunga magoli mengi kwenye ligi ya  Bundesliga.

Lewandowski ambaye kwa sasa maejiunga na klabu ya Barcelona kwenye dirisha la majira ya joto, amefanikiwa kuifungia klabu hiyo magoli 14 kwenye michezo 13 akiwa chini ya kocha Xavi.

Acha ujumbe