Mchezaji wa zamani wa Liverpool na sasa Bayern Munich Sadio Mane ametwaa tuzo ya Socrates kwenye tuzo za Ballon D’OR zilizokuwa zinatolewa hapo usiku wa jana nchini Ufaransa.

Sadio Mane ambaye ni raia wa Senegal ametwaa tuzo hiyo ambayo hutolewa kwa mchezaji ambaye amejitoa sana kwenye jamii yake, ambapo mchezaji huyo amekluwa akiisaidia jamii katika mambo mbalimbali kama vile kujenga hospitali na kutoa misaada mashuleni.
Mchezaji huyo amekuwa ni mtu ambaye hujali sana watu wa nchi yake, huku akipendelea maisha ya kawaida, huku akiangali alipotokea na kurejesha kati ya kile anachokipata kwenye jamii si jambo la kushangaza kwake.

Mane kwenye wachezaji watano bora Tuzo za Ballon D’OR ameshikilia nafasi ya pili huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Karim Benzema, Nafasi ya tatu imeenda kwa Kevin De Bruyne, nambari nne ni Roberto Lewandowski na Tano bora ni Mohamed Salah.

