Rais wa klabu ya Yanga Eng Hersi Said amesema mkakati mkubwa wa klabu hiyo kwasasa ni khakikisha wanatinga katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika.eng hersi saidKlabu ya Yanga baada ya kutupwa nje katika ligi ya mabingwa Afrika na klabu ya Al-Hilal kutoka nchini Sudan, Kwasasa wamepangwa na Club Africain kutoka nchini Tunisia kwenye mchezo wa mtoano ili kufuzu hatua ya makundi kwenye kombe la Shrikisho Afrika.

“Nataka niwahakikishie tutasonga mbele kwenda hatua ya Makundi [Shirikisho]. Usiipende Yanga kisa inashinda ikifungwa siyo yako. Tunapaswa kuwa na mapenzi na klabu hii na siyo mapenzi na matokeo, kama ni hivyo katafute kitu kingine cha kupenda.”Alizungumza Eng Hersi Said.eng hersi saidManeno hayo ameyazungumza Rais wa klabu ambapo Yanga tayari wanajiandaa kucheza mchezo huo na klabu hiyo kutoka Tunisia Novemba 2 ndani ya uwanja wa Benjamin Mkapa.

Pia Rais wa klabu hiyo Eng Hersi Said aliwataka mashabiki wa klabu ya Yanga kusimama na klabu yao muda wote na kuepuka kua mashabiki wa matokeo tu au pale timu inapofanya vizuri.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa