Cristiano Ronaldo ameelezea kurejea kwake Manchester United kama ‘janga’ katika madai mapya ya kushangaza kutoka kwenye kitabu kipya kinachokaribia kutolewa hivi karibuni,  huku kukiwa na uvumi unaoongezeka juu ya mustakabali wake Old Trafford.

Nyota huyo wa Ureno alirejea Old Trafford majira ya joto yaliyopita baada ya kuwaacha Mashetani Wekundu mwaka 2009 kwa uhamisho wa paundi milioni 80 kwenda kwa miamba ya Hispania Real Madrid.

 

Ronaldo Urejeo Wake Janga Klabuni Hapo

Kurejea kwa Ronaldo, hata hivyo, haijawa rahisi na kitabu kipya kitakachotolewa mwezi ujao kimeeleza kusikitishwa kwa fowadi huyo kurejea kwake.

Kitabu hicho kinajulikana kwa jina la, Messi vs Ronaldo: One Rivalry, Two GOATs, and the Era That Remade the World’s Game ambacho kinaelezea kwa undani maisha yake mashuhuri kimefichua yote, kwa mujibu wa The Sun.

Kimefichua kwamba Ronaldo hakufurahishwa na kocha mkuu wa muda Ralf Rangnick, akikiri ‘hili ni janga’ kwa afisa mkuu katika hafla ya FIFA.

 

Ronaldo Urejeo Wake Janga Klabuni Hapo

Hilo ni moja tu ya mambo ambayo yameweka maisha magumu kwa Ronaldo tangu arejee, kwani alikasirishwa na ukosefu wa uwekezaji kwenye uwanja wa mazoezi wa Carrington, huku akikerwa sana kwamba klabu hiyo haijabadilika tangu kuondoka kwake zaidi ya miaka kumi iliyopita.

Zaidi ya yote, pia alionekana kushtushwa sana na kiwango cha kujitolea kwa wachezaji kubaki katika hali ya juu. Licha ya hayo yote, Ronaldo ndiye mfungaji bora wa United katika klabu hiyo msimu uliopita, akifunga mabao 24 katika michuano yote katika mechi 39, licha ya kwamba bado anaonekana kuchanganyikiwa.

Mambo yamekuwa mabaya zaidi msimu huu kwa Ronaldo kwani anaonekana kugombana na bosi mpya Erik ten Hag, kumaanisha kwamba fowadi huyo amewekewa kikomo cha muda wa kucheza, akishiriki mara 13 katika mashindano yote, hasa akitokea benchi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa