Klabu ya Liverpool na kiungo wa kimataifa wa Argentina anayekipiga klabu ya Brighton Hove and Albion kila kitu kipo sawa ni suala la muda tu kiungo huyo kujiunga na Vijogoo hao wa Anfield.
Klabu ya Liverpool imeshafikia makubaliano ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina kwani mchezaji huyo ameonesha nia ya kujiunga na klabu, Mpaka sasa majogoo wa Anfield wameshakubaliana maslahi binafsi na kiungo MacAllister kilichobakia ni kulipa ada ya uhamisho kwa Brighton tu.
Dalili za kiungo MacAllister kuondoka ndani ya Brighton zilionekana pale ambapo kocha wa klabu hiyo Roberto de Zerbi aliposema kua inawezekana akawakosa wachezaji wake muhimu ndai ya msimu huu, Huku majina kama MacAllister na Moises Caicedo yakiwa yametajwa.
Klabu ya Liverpool inaelezwa inataka kuharakisha zaidi usajili wa kiungo huyo mapema ndani ya mwezi huu ili kuepuka ushindani kutoka katika timu zingine, Timu tofauti tofauti zimekua zikimfuatilia MacAllister ikiwemo klabu ya Manchester United ambayo inahitaji kiungo.
Kiungo MacAllister amekua na msimu bora sana ndani ya klabu ya Brighton pamoja na timu ya taifa ya Argentina ambapo alikua moja ya wachezaji muhimu walioisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa dunia, Huku Liverpool nao wanahitaji kiungo mwenye ubora mkubwa na macho yao yameangukia kwa kiungo huyo fundi.

