Lookman Atua Na Fulham Kwa Mkopo.


Fulham wamemsajili mshambuliaji wa zamani wa Everton, Ademola Lookman kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka RB Leipzig ya Ujerumani.

Lookman, 22, anarejea sasa katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) baada ya kujiunga na Leipzig kutoka Everton kwa kima cha £22.5m mwanzoni mwa msimu wa 2019-20.

Kwa mujibu wa mchezaji huyo raia wa Uingereza, maamuzi ya kutua Fulham ni sababu ya kushawishiwa na kocha wa kikosi hicho, Scott Parker.

 

Lookman Atua Na Fulham Kwa Mkopo.

“Baada ya mazungumzo na Parker, nilikubali kurejea EPL. Kubwa zaidi ni uhusiano bora ambao umekuwepo kati yangu na yeye,” akasema Lookman.

“Ni mwanasoka mchanga aliye na kiu ya kukua kitaaluma. Nami nimeridhishwa na kiwango cha ubora wake. Ni furaha kubwa kwamba alikubali kujiunga nasi,” akasema Parker.

Katika msimu wake wa kwanza akiwa Leipzig, Lookman alipachika wavuni mabao matano kwenye mechi 11 za Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) tangu ajiunge kwa mkataba wa kudumu Leipzig mnamo Julai 2019.

 

Lookman Atua Na Fulham Kwa Mkopo.

Fulham ambao wamerejea katika EPL msimu huu, wamepoteza jumla ya michuano mitatu ya ufunguzi wa msimu huu na ujio wa Lookman ni mojawapo ya mikakati ya kusukwa upya kwa kikosi hicho chini ya Naibu Mwenyekiti, Tony Khan.

Khan aliwaomba radhi mashabiki wa Fulham kwa kichapo cha 3-0 walichopokea kutoka kwa Aston Villa mnamo Jumatatu uwanjani Craven Cottage.


Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!

Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!

Soma Zaidi

32 Komentara

    kapige kazi kijana juhudi zako ndo zitakazokukalisha katika nafasi nzuri

    Jibu

    Sio mbay kapige kazi

    Jibu

    Kambi popote kapige kazi

    Jibu

    Wakati wa Lookman kupambana tena ndani ya EPL, Welcome back

    Jibu

    Kila lakheri lookman kapambane utafanikiwa.

    Jibu

    Kijana anajituma..

    Jibu

    Kabige kazi Lookman kambi kokote kijana

    Jibu

    Lookman yupo vizuri na ilikua ndoto yake kuja kucheza Fulham tunategemea mengi kuyaona clabuni hapo

    Jibu

    Lookman karibu Fulham

    Jibu

    Kila lakheri look man kaoneshe kipaji chako ndani ya Epl

    Jibu

    Wakati wa look man sasa kupambana

    Jibu

    Nenda kafanye kazi kikubwa maslai

    Jibu

    Asante kwa nakala

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Welcome. Epl look man

    Jibu

    Kijana yupo vzuri

    Jibu

    Lookman apige kazi huko ndio panamfaa

    Jibu

    Asnt kwa taarif

    Jibu

    Sio mbaya hata hapo

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Lookman yuko vizuri sana

    Jibu

    Safi sana kijana

    Jibu

    Lookman ni mchezaji mzuri sana

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Lookman anawez kuipaisha fulham

    Jibu

    saf

    Jibu

    Kaz kaz lukuman

    Jibu

    Lookman piga kazi

    Jibu

    Nic

    Jibu

    Kila la kher lookman.

    Jibu

    Lookman kupambana tena ndani ya EPL

    Jibu

    Safi

    Jibu

Acha ujumbe