Manchester United na Newcastle United kuna uvumi umekuwa ukisambaa na kuwapa hofu mashabiki wa Uingereza kuwa ujio wa Christian Ronaldo hautaweza kuonekana kwenye runinga siku ya jumamosi, kutokana na sheria iliyokuwepo toka mwaka 1960.
Zuio la mechi kuchezwa saa tisa alasiri, ndilo linatapelekea mechi kutoonyeshwa ambalo kwa mara ya kwanza lilitolewa na mwenyekiti wa timu Burnley, Bob Lord miaka ya 60, ili kuzuia uwezekano wa mashabiki kusalia nyumbani.
Bob alipendekeza kuwa hakuna mechi itakayoonyeshwa kwenye runinga kuanzia saa nane na dakika arobaini na tano hadi saa kumi na moja na dakika arobaini na tano, kwenye vituo vyote vya runinga nchini Uingereza, sheria hiyo haikuweza kufanya kazi kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa uviko 19 sababu mashabiki hawakuruhusiwa kuingia viwanjani.

Ni jambo la kushangaza kuwa mashabiki wanaoishi nchini Uingereza hawataweza kuingalia mechi hiyo lakini zuio hilo halizuii sehemu nyingine za dunia kutoitazama mechi hiyo kupitia runinga.
Manchester United inayotarajiwa kuchezwa saa kumi na moja kwa saa za Afrika Mashiriki imekuwa kivutio kikubwa kote ulimwenguni kutokana na kurejea kwa mshambuliaji hatari Christian Ronaldo kwa mara ya pili akitokea Juventus.
Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.


