Manchester United Watuma Ofa ya Ttau kwa Mount

Klabu ya Manchester United imeripotiwa kutuma ofa ya tatu kwa kiungo wa klabu ya Chelsea raia wa kimataifa wa Uingereza Mason Mount baada ya ofa mbili za mwanzo kukataliwa.

Manchester United wameboresha ofa yao mpaka kufikia paundi milioni 50 na nyongeza ya paund milioni 5 jumla paundi milioni 55, Huku ikielezwa hiyo itakua ofa ya mwisho kwa mashetani hao wekundu kwa mchezaji huyo.manchester unitedMan United wanaamini ofa ya sasa itapokelewa licha ya klabu ya Chelsea kuwaeleza kua watamuachia Mason Mount kwa paundii milioni 60 na sio chini ya kiwango hicho kama ambavyo walieleza katika mazungumzo yao ya awali.

Mason Mount na klabu ya Manchester United mpaka sasa wameshakubaliana juu ya maslahi binafsi ya mchezaji huyo na mchezaji nae akionesha anahitaji kuondoka ndani ya viungo vya Stamford Bridge katika majira haya ya joto.manchester unitedManchester United wanaripotiwa kuhitaji kufanya haraka iwezekanavyo kwa mchezaji huyo ili wiki ijayo ikifika Mason Mount awe tayari ni mchezaji wa klabu hiyo kwani wana matumaini kua Mount ndio utakua usajili wao wa kwanza katika majira haya ya joto.

Acha ujumbe