Manchester United Yamuuza Kinda Wake

Klabu ya Manchester United yakubali kumuuza kinda wake raia wa kimataifa wa Iraq mwenye umri wa miaka 20 kwenda klabu ya Utrecht ya nchini Utrecht.

Manchester Unired imekubali kumuachia kinda huyo ambaye amekua akifanya vizuri kwenye timu ya vijana wa miaka 20 ambapo ilimfanya mpaka kujumuishwa kwenye timu ya kwanza ambapo amekua hapati nafasi mara kwa mara.manchester unitedKlabu ya Man United ipo kwenye utaratibu wa kuuza wachezaji ili iweze kununua wachezaji kwani bajeti ya klabu hiyo inakadiriwa kua paundi 120, Hivo klabu hiyo inategemea kuuza baadhi ya wachezaji ili kupata hela usajili.

Manchester United mpka sasa ipo sokoni ambapo mauzo ya klabu hiyo bado hayajakamilika na bado haijafafahamika yatakamilika lini, Kutokana na hali hiyo bajeti yausajili pia imekua ndogo na ndio sababu wanalazimika kuuza baadhi ya wachezaji.manchester unitedZidane Iqbal anaondoka ndani ya Manchester United akiwa kama kijana ambae alikua anatarajiwa kufanya makubwa ndani ya timu hiyo, Lakini ameuzwa kwenda klabu ya Utrecht huku wengi wakitarajia atarejea ndani ya klabu hiyo miaka ya mbeleni kama akifanya vizuri ndani ya timu yake mpya.

Acha ujumbe