Timu Samatta imefanikiwa kuifunga timu ya Alikiba yaani Team Kiba katika mchezo wa hisani uliopigwa katika dimba la Chamazi leo kwa mabao manne kwa mawili.
Timu Samatta wameweza kulipiza kipigo ambacho walikipokea mwaka jana katika mchezo huu wa hisani ambapo Timu Kiba walifanikiwa kushinda kwa mikwaju ya penati, Lakini mwaka huu wamekataa uteja na kuweza kuibuka kidedea.Mabao ya matatu ya Abdul Sopu na bao moja la John Bocco yaliweza kuipatia ushindi timu Samatta leo, Huku upande wa kiba mabao yao ya kufutia machozi yakifungwa na Ruben Lyanga pamoja na msanii Marioo.
Mchezo huo wa hisani ambao unapigwa kwa msimu wa sita umekua una lengo la kuhakikisha wanarudisha kwenye jamii yao, Kwani watu wote wawili ambao wameandaa mchezo ni watu wenye ushawishi hivo huandaa mchezo huo kwajili ya kusaidia jamii zaidi.Mwaka huu mchezo wa Timu Samatta na Timu Kiba ulikua una kaulimbiu ya “Upendo wa Dhambarau Simama na Mtoto Njiti” Kampeni ya mwaka huu ilikua inalenga zaidi kuhakikisha inasimama na watoto ambao wanazaliwa kabla ya umri hivo hela zote zitakazopatikana kwenye kampeni hii zitakwenda kusimama na watoto Njiti.