Klabu ya Borussia Dortmund inafikiria kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial endapo watamuuza mshambuliaji wao Erling Haaland katika majira yajayo ya kiangazi.

Mkataba wa Haaland wa sasa unakipengele ambacho kitamfanya kuuzwa kwa bei ndogo ya Euro 75 mil kuanzia majira ya kiangazi mwaka 2022.
Martial anaangaliwa kama mbadala mzuri wa mshambuliaji huyo baada ya kukosa namba katika kikosi cha kwanza cha Ole Gunnar Solskjaer hasa baada ya kurejea kwa mshambuliaji wao wa zamani Cristiano Ronaldo.
Martial amebakiza miaka 3 katika mkataba wake wa sasa ambao unatarajiwa kukamilika mwezi juni mwaka 2024, Dortmund wanaweza kuwashawishi United kumuuza mchezaji huyo endapo watatoa dau zuri kwaajili ya kumsajili mchezji huyo.
Ni wakati wa ushindi mkubwa ukiwa na kasino bomba ya Lock a Luck, meridianbet wanakupa sababu ya ushindi, funga bahati yako ya ushindi ukiwa na mabingwa.



Sania+mapua
Itakuwa poa tu