Mcheza Tennis kinda wa Uingereza, Emma Raducanu 18, ameacha rasmi kufanya kazi na kocha wake Andrew Richardson wiki chache baada ya kushinda taji la US Open kwa mara ya kwanza.

Kocha Richardson alikuwa kocha wa Raducanu katika kituo cha Tennis cha Bromley Centre kabla ya kuchaguliwa kusindikiza mchezaji huyo katika mashindano ya US Open kwasababu ya kufahamiana.
“Nilipokuwa nafasi ya 200 kabla ya mashindano ya Wimbledon na muda ule nilidhani Andrew [Richardson] angekuwa kocha mzuri lakini hatukufanikiwa, nilikuwa na ndoto za kushinda US Open na nimefanikiwa, nipo nafasi ya 22 duniani ambayo ni hali ya kustaajabisha kwangu.” alisema Raducanu.
“Nadhani katika ngazi hii ya kazi yangu na kucheza na wachezaji wakubwa duniani, nimegundua nahitaji mtu ambaye ana uzoefu wa kiwango cha WTA., nikimaanisha mtu ambaye yupo katika ngazi anayojua ninahitaji nini kufika pale.
“Hasa wakati huu ambao ni mgeni katika nafasi hii, nahitaji mtu ambaye anaweza kuniongoza ambaye aliwahi kupitia huko.” aliongeza.
Ni wakati wa ushindi mkubwa ukiwa na kasino bomba ya Lock a Luck, meridianbet wanakupa sababu ya ushindi, funga bahati yako ya ushindi ukiwa na mabingwa.


