Klabu ya Simba SC leo itashuka katika Uwanja wa Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro majira ya saa kumi kamili jioni kuikabili Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Katika mchezo huo wa pili wa ugenini Simba SC wanataraji akuondoka na ushindi baada ya kufanya hivyo katika dakika za mwisho katika mchezo wa mwisho dhidi ya Costal Union ya Tanga.

 

simba sc, Matchday : Polisi Tanzania vs Simba SC, Meridianbet

Kocha wa Simba SC, Pablo Franco amesema licha ya ugumu wa ratiba ambayo inawafanya kukosa muda wa kutosha kujiandaa kutoka mechi moja hadi nyingine lakini watapambana kupata alama tatu.

“Mchezo utakuwa mgumu zaidi kwetu, hatujapata muda wa kufanya mazoezi. Tumesafiri juzi kwa basi kuja hapa tukitoka Tanga jana wachezaji wamefanya mazoezi na leo mechi, kwa hiyo hatujapumzika. Lakini tutapambana,” alisema Pablo.

Baada ya mchezo huo Simba SC itarejea jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini utakaopigwa Jumapili ijayo majira ya saa moja jioni.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa