Mchezaji wa Manchester City, Benjamin Mendy (27) sasa anashtakiwa kwa makosa nane ya ubakaji, shtaka moja la unyanyasaji wa kijinsia na moja la kujaribu kubaka na hii ni baada ya mwathiriwa mpya kujitokeza.

Mnamo mwezi uliopita, Mendy alikana mashtaka yote isipokuwa shtaka la hivi karibuni la kujaribu kubaka ambalo anatarajiwa kulijibu Julai 25, 2022.
Makosa yote yanadaiwa kutendeka nyumbani kwa mchezaji huyo kati ya Oktoba 2018 na Agosti 2021.
Mendy, ambaye amecheza mechi 50 za Premier League akiwa na Manchester City tangu ajiunge nayo akitokea Monaco mwaka 2017 na amecheza mechi 10 za kimataifa akiwa na Ufaransa, alisimamishwa na klabu hiyo baada ya kushtakiwa.
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!


