Mchezaji wa Juventus Arek Milik mwenye umri wa miaka 28 na anayecheza katika nafasi ya kiungo wa mbele hajashiriki katika mazoezi ya asubuhi ya leo huko Continassa kutokana na tatizo la misuli.

 

Milik( 28) Kuwakosa Maccabi Haifa

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Poland hakuhusika katika mazoezi ya asubuhi ya leo katika mkesha wa mechi muhimu ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Maccabi ya Israel kesho. Hakufanya mazoezi uwanjani, lakini alifanya kazi kwenye gym tu kutokana na uchovu wa misuli.

Juventus wamepoteza michezo miwili kati ya mwanzo kwenye ufunguzi wa michuano hiyo na wanatamani sana kupata ushindi ambao utawapa matumaini yao ya kufuzu kwenda hatua inayofuata ya 16 bora.

Milik ni mmoja wa wafungaji bora wa Juventus msimu huu, akiwa na mabao manne katika mechi saba katika michuano yote, likiwemo moja la Ligi ya Mabingwa dhidi ya Benfica mwezi uliopita.

Milik( 28) Kuwakosa Maccabi Haifa

Football Italia inaelewa kuwa tatizo la Milik la misuli halipaswi kuwa kubwa sana, lakini kocha wa klabu hiyo Massimiliano Allegri atatoa taarifa za hivi punde kuhusu upatikanaji wa mshambuliaji huyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kabla ya mechi hiyo kesho.

Milik alijiunga na Juventus kutoka Marseille msimu wa joto kwa mkopo na chaguo la kumnunua kwa Euro Milioni 7. Mshambuliaji huyo  wa zamani wa Napoli alifunga mabao 48 katika michezo 122 katika kipindi chake cha miaka minne na nusu huko Naples.

Milik( 28) Kuwakosa Maccabi Haifa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa