Kocha wa klabu ya Fc Barcelona ya nchini Hispania Xavi ameeleza kua hafikirii suala la kulipa kisasi katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya utakaofanyika katika dimba la San Siro usiku wa leo timu yake itapokutana na klabu ya Interzionale Milan.
Klabu ya Fc Barcelona leo usiku itakaribishwa katika dimba la San Siro na klabu ya Inter Milan ambao ndo wenyeji wa mchezo huo ambapo mchezo wa mwisho klabu hiyo kufika katika dimba hilo ilikua nusu fainali wa ligi ya mabingwa barani ulaya msimu wa 2009/10 ambapo Barcelona waliambulia kipigo cha mabao matatu kwa moja na kutolewa kwenye michuano na wenyeji wa mchezo huo.
Katika mchezo ambao ulikua unatazamiwa kama kisasi kwa kocha wa timu hiyo Xavi baada ya kufika hapo mara ya mwisho na kupokea kipigo lakini imekua tofauti kwa kocha huyo na kusema “Sifikirii kuhusu kulipa kisasi. Nimekuja hapa kama kocha wakati huu. Nakumbuka tulisafiri na basi hadi Milan kwasababu ya volcano lakini ilikua timu nzuri”
“Ulikua mchezo mgumu kwetu kwenye mzunguko wa kwanza. Na tulipoteza hapa. ulikua mchezo wa utata kidogo,ila ndivyo ilivyokua na ni kumbukumbu ngumu kwetu kiukweli”Alisema Xavi.
Kocha huyo ameeleza wamejikita zaidi kupata alama tatu muhimu ili kujiwekea mazingira mazuri kufuzu hatua ya 16 bora kuliko kulipiza kisasi hii ni baada ya kutoka kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Bayern Munich katika dimba la Allianz Arena.
Kocha huyo ameeleza pia ukubwa wa mpinzani wake anachofikiri ni kutawala mchezo huo kwasababu ni michuano ya ulaya na sio mchezo mwepesi , Hivo mchezo muhimu ambao utakua umeshikilia hatma ya kundi hilo.