Kocha mkuu wa Al Ahly Pitso Mosimane amefunguka kuwa moja ya mechi ngumu zaidi kuwahi kucheza katika msimu huu ni ile ya ugenini dhidi ya Simba katika hatua ya makundi ya CAF Champions League.
Katika mahojiano ya mwisho na mwanahabari wa Misri, Mosimane alieleza kinaga ubaga namna ambavyo kipigo kutoka kwa timu ya Simba pale kwa Mkapa kiliwafanya waamke na kuamua kubadili baadhi ya Vitu.
Kauli hizo zilitolewa saa chache tu baada ya Ahly kuchukua ubingwa wa Afrika kwa kuichapa timu ya Kaizer Cheifs kutoka South Afrika ambayo ndiyo iliyoiondoa Simba kwenye hatua ya Robo fainali.
Simba ilikuwa mwakilishi pekee wa klabu bingwa Afrika kwa upande wa Tanzania lakini msimu ujao, Tanzania itatoa timu mbili kuelekea michuano hiyo mikubwa itakayoanza kushuka hatamu mwezi septemba.
KASINO YA MAYAN EAGLE INAKUKUFANYA KUWA BINGWA WAKATI WOWOTE UNAPOAMUA KUICHEZA. UTABURUDIKA HUKU UKIENDELEA KUTENGEZA MKWANJA MREFU, JIUNGE SASA NA UWE MIONGONI MWA MABINGWA!!
Sarah
Simba baba lao