Moyes Aionya Westham Kuwa Kazi Bado Haijaisha.

Kocha wa West ham David Moyes amefurahi kuona West Ham ikifuzu kwa hatua ya mtoano ya UEFA Europa Conference League lakini akaionya timu yake kuwa kazi bado haijakamilika baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Anderlecht.

 

Moyes Aionya Westham Kuwa Kazi Bado Haijaisha.

Wagonga nyundo wa London hao waliwashinda wapinzani wao wa Ubelgiji wanaocheza ligi ya Pro League kwenye Uwanja wa London Stadium hapo jana, ambapo mabao hayo yalitupiwa kambani na Said Benrahma na Jarrod Bowen, katika mechi iliyokumbwa na mvurugano ndani ya uwanja.

Ushindi huo unaimarisha zaidi nafasi ya West Ham kileleni mwa Kundi B kwa kushinda mechi nne zote za mwanzo  Lakini kutokana na timu zilizomaliza katika nafasi ya kwanza na kutinga hatua ya 16 bora, na washindi wa pili kulazimika kujiandaa kwa awamu ya mchujo na timu kuondolewa kwenye Ligi ya Europa, Moyes alionya kwamba bado kuna kazi ya kufanywa.

Moyes Aionya Westham Kuwa Kazi Bado Haijaisha.

“Nimefurahishwa sana kuwa tumefuzu kwa hatua inayofuata,” alisema. “Jambo kubwa ni kuwa Ulaya kila wakati baada ya Krismasi.

Moyes aliwagusia Silkeborg na kusema kuwa timu hiyo inaonekana kuwa tatizo kwao  kutokana na mabao wanayofunga, kwa hivyo bado tunahitaji pointi ili kuwa washindi wa kundi na wanatumaini kuwa wanaweza kufanya hivyo lakini kushinda usiku wa jana ilikuwa muhimu na walistahili kushinda lakini waliifanya kuwa ngumu zaidi kwao kuliko ilivyopaswa kuwa.

Moyes na vijana wake baada ya michuano hiyo, Wikendi hii watashuka dimbani kukipiga dhidi ya Southampton wakiwa ugenini huku mechi iliyopita wagonga nyundo hawo wametoka kushinda kushinda ushindi mzuri.

Moyes Aionya Westham Kuwa Kazi Bado Haijaisha.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.