Meneja wa West Ham, David Moyes amemshutumu meneja mwenza wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer kumzuia kiungo Jesse Lingard Kurejea kwa wagonga nyundo hao.

Jesse Lingard akichezea West Ham kwa mkopo msimu uliopita na klabu hiyo ilijaribu kumsajili akitokea united kwa mkataba wa kudumu katika dirisha la usajili lililopita.
“Ole aliweka wazi kwangu, mapema sana kabla ya dirisha la usajili kuanza kwamba anahitaji abaki katika timu hiyo, alisema Moyes.
” Kwahiyo nilijua vizuri mapema kwamba katika dirisha la usajili atabaki Manchester United. Nilikuwa na maongezi binafsi pamoja na Ole aliweka wazi kwamba atabaki.”
Lingard akiwa chini ya Moyes msimu uliopita kuanzia January 2021 amefanikiwa kucheza mechi 16 akifunga magoli 9 na ku assist mengine 4.
Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!


