Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Barcelona ina mpango wa kujaribu kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa England na Manchester City Raheem Sterling, 26, mwezi Januari baada ya kushindwa kumleta Nou Camp majira ya joto.

Ajenti wa Paul Pogba Mino Raiola anasema kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 28-huenda akajiunga tena na Juventus wakati mkataba wake na Manchester United utakapomalizika mwisho wa msimu huu.

Mshambuliaji wa Inter Miami Gonzalo Higuain anasema klabu hiyo ya MLS ina ndoto ya kumsajili Lionel Messi wakati mkataba wa nyota huyo na Paris St-Germain itakapomalizika mwaka 2023.

 

Tetesi zinasema, Liverpool wameanzisha mazungumzo ya kandarasi mpya na kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita,26. Kandarasi yake ya sasa inamalizika mwaka 2023.

Mhambuliaji Kayky, 18, raia wa Brazil ameanza kufanya mazoezi na Manchester City baada ya klabu hiyo kukamilisha uhamisho wake kutoka Fluminense, ambao awali ulikuwa ukamilishwe Januari.

Tetesi zinasema, huenda Tottenham wakafufua upya mpango wao wa kumsaka beki wa Ujerumani Antonio Rudiger mkataba wake na Chelsea usiporefushwa msimu ujao.

Tuchel amepuuzilia mbali tetesi kuwa Chelsea ilijaribu kumsajili mshambuliaji wa England Harry Kane, 28, kutoka Tottenham, lakini akasema alitarajia atajiunga na Manchester City.

Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta anasema mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 30- Alexandre Lacazette, ambaye kandarasi yake inamalizika msimu ujao, atakuwa kiungo muhimu kwa kikosi chake msimu huu.

 

Tetesi zinasema, winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, 20, anafiria kubadili uraia wake wa kimataifa kutoka England na kwenda Ghana.

Tetesi zinasema, Kocha wa Burnley, Sean Dyche ana matumaini wachezaji kadhaa watasalia katika klabu hiyo kufuatia hatua yake ya kusaini kandarasi mpya.

Mlinzi wa Uhispania Sergi Roberto, 29, atasaini kandarasi mpya na Barcelona wiki chache zijazo baada ya kufikia mkubaliano na rais wa klabu hiyo Joan Laporta.


MKWANJA NJE NJE NA DISCO FUNK

Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe