Kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amempagawisha Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji kutokana na mbinu alizotumia kuvuka hatua ya awali ya mashindano ya Klabu bingwa barani Afrika.

 

Nabi Ampagawisha Bosi Yanga

Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 9-0 dhidi ya Zalan FC kwenye mchezo wa hatua ya awali ya mashindano hayo.

Akizungumzia hilo, Arafat alisema kuwa “Mwaka jana tulikosa nafasi ya kuvuka hatua hii kutokana na kuwakosa baadhi ya wachezaji wetu na pia tulikuwa tunaiandaa timu yetu.

“Kwa msimu huu mambo yamekuwa mazuri kwetu na wachezaji tuliokuwa nao msimu uliopita hawajabadilika sana hivyo imeongeza kitu kwenye timu.

“Kila mmoja alikuwa na hofu baada ya kile kipindi cha kwanza matokeo kutopatikana lakini nawapongeza benchi la ufundi likiongozwa na Kocha Nabi kwa kuusoma mchezo na katika kipindi cha pili timu kupata matokeo.”

 

Nabi Ampagawisha Bosi Yanga

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa