Mshambuliaji mpya wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa Christopher Nkunku anatajwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki kumi na sita.
Mshambuliaji Nkunku amepata majeraha ya goti na atakwenda kufanyiwa upasuaji ambao utamuweka nje ya uwanja kwa muda wa wiki 16 ikiwa ni taarifa mbaya sana kwa upande wa klabu ya Chelsea.Mchezaji huyo ambaye ameonekana kufanya vizuri kwenye michezo ya kujiandaa na msimu mpya, Hivyo kupata kwake majeraha makubwa kutapelekea kuifanya klabu ya Chelsea kukosa huduma bora ya mchezaji huyo.
Mchezaji Nkunku ambaye alikua mfumgaji bora wa ligi kuu ya Ujerumani na kufanya vizuri ndani ya klabu hiyo kabla ya kujiunga na klabu ya Chelsea ambapo alitarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji wa klabu hiyo.Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekua na mwendelezo wa majeraha mara kwa mara, Kwani hata mwaka jana mwishoni alishindwa kushiriki michuano ya kombe la dunia na timu ya taifa ya Ufaransa kwajili ya majeraha.