Klabu ya Manchester United iko mawindoni kumsajili beki wa katikati raia wa kimataifa wa Ufaransa Jean Clair Todibo anayekipiga klabu ya Nice ya nchini Ufaransa.
Manchester United wapo kwenye mikakati ya kutafuta beki wa kati mwenye ubora wa hali ya juu kwakua wanataka kuachana na Harry Maguire, Hivo Todibo inaelezwa ndio chaguo sahihi kwa kocha Ten Hag mpaka sasa.
Mashetani wekundu wameshafanikiwa kusajili wachezaji watatu ambao ni Mason Mount, Andre Onana na mshambuliaji Rasmus Hojlund na kwasasa mipango yao imehamia kwa kiungo Sofyan Amrabat pamoja beki Jean Todibo.
Man United imekataa ofa ya klabu ya West Ham ya paundi milioni 60 kwajili ya kuwasajili wachezaji wake Harry Maguire pamoja Scott Mctominay, Huku wakihitaji pesa zaidi ya hiyo ili waweze kupata saini ya wachezaji wanaowataka sokoni na wao.
Beki Jean Todibo ambaye amewahi kupita klabu ya Barcelona amekua akifanya vizuri kwa klabu ya Nice ya nchini Ufaransa akiwa ni moja ya mabeki vijana wanaowafanya vizuri kwenye ligi hiyo jambo liliwavutia klabu ya Manchester United kutaka kumsajili.

