Meneja wa Real Betis, Manuel Pellegrini amesema La Liga inatia aibu kwa kuwa nyepesi sana na anasema lazima wafanye juhudi kupunguza matukio ya kupoteza muda na kujidondosha.
Kocha huyo wa Chile alishuhudia timu yake ya Real Betis ikilazimishwa sare ya bao 1-1 na Cadiz katika pambano lao la ligi siku ya Ijumaa.
Pellegrini alisikitishwa na timu yake kushindwa kupata ushindi dhidi ya wapinzani wao waliokuwa wanajihami (kupaki basi), pia anaamini timu kubwa za ligi hiyo zinarudishwa nyuma na timu zinazoharibu flow ya mchezo.
Pellegrini alianzisha harakati katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya mechi, akiwaambia waandishi wa habari:
“Lazima tufanye juhudi kati ya waamuzi, makocha na wachezaji ili La Liga isiwe aibu, kwasababu katika mkutano wa waamuzi walituambia kwamba ni ligi ya polepole zaidi barani Ulaya.
“Watu wanataka kutazama mchezo mzuri, na hatuwapi. Kupoteza muda na kujidondosha ni aibu.
“Kuna michezo ambayo inapaswa kuitunza. Mashabiki wanalipia tiketi kupata kitu.”
Ni muda wa kuwa milionea na kasino za mtandaoni za meridianbet, mchezo wa Sahara Riches unakupa nafasi ya kushinda mkwanja mrefu. Matajiri wa jangwani wanataka wakupe mkwanja leo.
Sarah
Duuh