Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesisitiza kiungo wa klabu hiyo Paul Pogba hataondoka Old Trafford kwenye dirisha la uhamisho la majira ya kiangazi.

Pogba anaendelea kuhusishwa na kuondoka Old Trafford wakati Paris Saint-Germain ikiripotiwa kumtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa.
Mchezaji huyo yupo mwaka wa mwisho wa mkataba wake na United, Solskjaer alisema mnamo Julai kuwa klabu hiyo ilikuwa katika mazungumzo ya kumpa mkataba mpya wa muda mrefu.
“Ndio, ninatarajia Paul atakuwa hapa wakati mwezi Septemba utakapoanza,” Solskjaer aliwaambia waandishi wa habari.
“Ikiwa una kandarasi ya miaka mitano au kandarasi ya mwaka mmoja, wakati unasaini Man Utd lazima upate changamoto ya kufanya kwa kiwango sawa.
“Sina wasiwasi wowote kwamba urefu wa mkataba kwa mchezaji yeyote unabadilisha kiwango cha motisha na kiwango chake. Unatakiwa kucheza vizuri kwa timu yako, wachezaji wenzio, wewe mwenyewe, na familia yako, kila wakati unapocheza.
“Ninatarajia kwamba mtazamo wa kila mchezo ndio sahihi. Kwamba tunazingatia mwelekeo sahihi, taaluma sahihi na, pamoja na hayo, sina wasiwasi wowote juu ya Paul. ” aliongeza.
Ni muda wa kuwa milionea na kasino za mtandaoni za meridianbet, mchezo wa Sahara Riches unakupa nafasi ya kushinda mkwanja mrefu. Matajiri wa jangwani wanataka wakupe mkwanja leo.



Sarah
Vizuri