Pioli Anatarjia Ushindani Mkubwa Dhidi ya Spurs

Kocha wa klabu ya Ac Milan Stefano Pioli aliridhishwa na matokeo ya bao moja kwa bila klabu yake iliyoyapata katika mchezo wa hatua ya 16 bora jana usiku dhidi ya Tottenham Hotspurs lakini akitarajia mtihani mzito katika mchezo wa marudiano.

Bao la mapema la kiungo Brahim Diaz lilihakikisha klabu ya Ac Milan inakua na faida katika mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa ulaya utakaopigwa jijini London Manchi 8, Baada ya ushindi huo kocha Pioli alionesha kuridhika na matokeo hayo lakini pia ameweka wazi anaelewa kabisa ugumu atakaokutana nao katika mchezo wa marudiano.PioliKlabu ya Ac Milan ambao ni mabingwa mara saba wa ligi ya mabingwa barani ulaya wamefanikiwa kupata alama tatu jana dhidi ya klabu ya Tottenham Hotspurs wakiwa katika dimba lao la nyumbani San Siro, Huku ikiwa ni muendelezo mzuri wa klabu hiyo baada ya kupata matokeo ya ushindi kwa mechi ya pili mfululizo.

Kocha Pioli amezungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo dhidi ya Tottenham na kusema “Ilikua mechi ngumu na ngumu dhidi ya timu ngumu. Tulicheza mchezo mzuri, Lakini najua mchezo ujao utakavyokua mgumu, Ila kwa leo nimeridhikaPioliKocha Stefano Pioli ambae amepitia kipindi kigumu wiki kadhaa zilizopita kutokana na klabu ya Ac Milan kufanya vibaya katika michezo yake, Lakini klabu hiyo imefanikiwa kupata matokeo katika michezo yake miwili ya mwsho kitu ambacho kocha huyo anaamini kinaweza kurudisha ari ya timu hiyo.

 

Acha ujumbe