Pioli Ajitetea Kutosajili Golikipa

Kocha wa klabu ya Ac Milan inayoshiriki ligi kuu ya Italia Stefano Pioli amejitetea baada ya kutosajili golikipa kwenye dirisha dogo licha ya golikipa wake namba moja kukosekana kwa muda mrefu.

Klabu ya soka ya Ac Milan kwasasa inamkosa golikipa wake namba moja Mike Maignan tangu mwezi Septemba mwaka jana akiwa anaitumikia timu yake ya taifa ya Ufaransa dhidi ya Austria, Lakini haijajulikana lini golikipa huyo lini atarudi kwenye lango la Ac Milan.PioliTaarifa zinaeleza kua bodi ya wakurugenzi ya klabu ya Ac Milan ndio ilipiga chini mpango wa kusajili golikipa mpya ndani ya timu hiyo, Lakini kocha Pioli amesema sio suala la bodi ni yeye pamoja na benchi la ufundi walikubaliana kutokusajili golikipa mwingine katika dirisha dogo la mwezi Januari.

Kocha Stefano Pioli amesema kua klabu hiyo ina imani na golikipa wake mkongwe Ciprian Tatarusanu ambaye ndio amekua akikaa kwenye lango la AC Milan tangu kuumia kwa golikipa wake namba Mike Maignan ambaye haijafahamika ni lini atarejea katika timu hiyo.PioliKocha huyo amezungumza hayo kuelekea mchezo wao wa ligi kuu nchini humo dhidi ya klabu ya Torino, Vilevile kocha Pioli aliulizwa kuhusu kurejea kwa golikipa wake Maignan na kujibu kua hana uhakika lini atarejea lakini akikiri kua anaendelea vizuri lakini bado hajarejea kufanya mazoezi na timu.

Acha ujumbe