Meneja wa Manchester United, Ralf Rangnick amesifu kiwango cha mshambuliaji Marcus Rashford baada ya timu yake kupata ushindi wa dakika za lala salama dhidi ya West Ham.
Bao la dakika za lala salama lililofungwa na Rashford linafanya kuwa ushindi wa pili mfululuzo kwa Rangnick na kurejea nafasi ya nne kwa kuwaondoa West Ham.
“Ni mmoja wa washambuliaji bora EPL,” alisema Rangnick. “Ni mchezaji wa kimataifa wa Uingereza, ambaye alicheza mara kwa mara kwenye Euro na sote tunajua ana ubora gani.
“Ana karibu kila kitu ambacho mshambuliaji wa kisasa anahitaji. Ana kasi, ujuzi, ana ukubwa na umbile la mshambuliaji na mwishowe ni kujiamini kwa washambuliaji.
“Nina uhakika kwamba mabao hayo mawili yameongeza kiwango cha kujiamini ndani ya Marcus lakini sasa ni juu ya kuchukua hatua, kuonyesha hilo mara kwa mara.
“Ni juu ya mwendelezo sasa na nadhani anaweza kuchukua jukumu muhimu sana kwa msimu uliobaki kwetu.” aliongeza.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.