Nahodha wa klabu ya Chelsea Reece James imeelzwa amepata majeraha katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Liverpool wikiendi iliyomalizika.
Reece James ambaye ametangazwa kama nahodha mpya wa klabu ya Chelsea siku kadhaa nyuma, Lakini pigo kwa klabu ya Chelsea ni taarifa ya beki huyo kupata majeraha ya nyama za paja.
Beki huyo raia wa kimataifa wa Uingereza baada ya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya Liverpool haikuzaniwa kama itakua hatari kwa kiwango hicho, Kwani hata kocha wa timu hiyo Mauricio Pochettino alieleza sio majeraha makubwa.
Taarifa za majeraha ya beki huyo ambazo zimetoka rasmi leo na haijawekwa wazi atakua nje ya uwanja kwa muda gani, Lakini mara nyingi majeraha ya misuli ya nyama za paja mara nyingi huwaeka wachezaji nje kwa muda kidogo.
Klabu ya Chelsea imeanza kuonja uchungu wa majeraha msimu huu ambao umekua ukiandama timu nyingi kwa siku za karibuni baada ya Reece James majeraha, Huku hofu kubwa ni kwa beki huyo ambaye amekua akipata majeraha ya mara kwa mara.

