Reece James Nahodha Mpya Chelsea

Beki wa kulia wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza Reece James ametangazwa kua nahodha mpya wa klabu hiyo kuelekea msimu ujao wa mwaka 2023/24.

Reece James ametangazwa kua nahodha wa Chelsea akichukua mikoba ya aliyekua beki mkongwe wa klabu hiyo Cesar Aziplicueta ambaye ametimka klabuni hapo na kutimkia klabu ya Atletico Madrid ya nchini Hispania.reece jamesBeki huyo wa kimataifa wa Uingereza licha ya umri wake mdogo lakini ameweza kuaminiwa kuongoza jeshi la Chelsea, Huku pia kukiwa na wachezaji wengine wakongwe ndani ya timu hiyo kama beki wa kimataifa wa Brazil Thiago Silva.

Beki huyo wa kulia amekua akionesha uwezo mkubwa tangu alipopewa nafasi kwenye timu ya wakubwa kwa mara ya kwanza akitokea klabu ya vijana ya timu na aliyekua kocha wa klabu hiyo Frank Lampard.reece jamesBeki Reece James ni mchezaji ambaye amekuzwa katika akademi ya klabu ya Chelsea inayofahamika kama Cobham, Hivo kutokana na ubora ambao anauonesha ndani ya kikosi hicho wakati huohuo ni Chelsea asilia imempa nafasi kubwa ya kuvaa kitambaa cha unahodha klabuni hapo.

Acha ujumbe