Ruben Amorim: “Tulikuwa Tunapata Wakati Mgumu"

Ruben Amorim amekiri kuwa timu yake ya Manchester United ilikuwa ikijaribu tu “kuhimili presha” kipindi cha pili baada ya kuwekwa chini ya shinikizo kubwa na Newcastle United.

Ruben Amorim: “Tulikuwa Tunapata Wakati Mgumu"

Mashetani Wekundu walipata bao la uongozi pale mpira wa mkwaju mkali wa Patrick Dorgu ulipopita kwa Aaron Ramsdale. Bao hilo hatimaye lilitosha kuwapatia wenyeji pointi zote tatu, ingawa walilazimika kujilinda kwa nidhamu kubwa ili kuhakikisha wanadumisha ushindi huo.

Licha ya Newcastle United kutawala umiliki wa mpira kwa sehemu kubwa ya kipindi cha pili, walishindwa tena kuvunja safu imara ya ulinzi na wakaondoka Old Trafford wakiwa wamepata tena kipigo cha ugenini kwenye Ligi Kuu.

The Magpies wamekusanya pointi sita tu kati ya 27 zinazowezekana wakiwa ugenini kwenye ligi msimu huu, na ni Wolves pekee walioko mkiani mwa msimamo wa ligi wenye ushindi mdogo zaidi wa ugenini kuliko kikosi cha Eddie Howe.

Ruben Amorim: “Tulikuwa Tunapata Wakati Mgumu"

Baada ya ushindi huo wa jana vijana wa Amorim hadi sasa wamesogea hadi nafasi ya 5 huku wakiwa pointi sawa na The Blues ambaye yupo nafasi ya 4 lakini wao wapo mbele mchezo mmoja. Pia wapo nyuma pointi 10 kwa kinara wa ligi.

Mechi inayofuata ya ligi Manchester United chini ya Amorim watakuwa nyumbani pia kumenyana dhidi ya Wolves ambao mpaka sasa ndio vibonde wa ligi wakiwa na pointi zao 2 pekee.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.