Huku dirisha la Usajili Duniani likiwa limefungwa kwa baadhi ya vilabu vingi Duniani, kuna sajili nyingi za gharama mbalimbali zimefanyika kutokana na Ligi huku ligi pendwa ikiwa ndio inashika kinara.
Pale EPL umefanywa usajili mkubwa sana kwenye vilabu mbalimbali huku kwa ujumla klabu ambayo imeongoza kwa matumizi ya pesa nyingi kwenye usajili ikiwa ni Chelsea lakini timu ambayo imesajili mchezaji wa gharama ikiwa ni Arsenal ambayo imemsajili Declan Rice kwa shilingi B 312 kutoka West Ham.
Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.
Usajili mwingine wa gharama umefanywa kule LALIGA na klabu ya Real Madrid ambayo imemsajili Jude Bellingham kwa shilingi B 277.8 kutoka klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani na mchezaji huyo anaendelea kufanya vizuri ambapo amepachika mabao sita hadi sasa kwenye michezo minne aliyocheza.
Usajili wa tatu wa gharama umefanywa pale BUNDESLIGA katika klabu ya Bayern Munich ambayo wao wamemsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Tottenham Hot Spurs Harry Kane kwa B 269.7 Tsh huku wakitegemea awe mrithi wa Roberto Lewandowski aliyetimkia FC Barcelona msimu uliopita.
Pia pale tukihamia jiji la starehe Ufaransa, LIGUE 1 ambapo PSG wamemsajili Randal Kolo Muani kwa shilingi B 256.2 kutoka Eintracht Frankfurt ya Ujerumani. Huo ukiwa ni usajili wa gharama uliofanywa kuliko vilabu vyovyote hapo.
Ukiwa na meridianbet odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.
Kule kwa matajiri sasa Saudi Arabia katika klabu ya AL-Hilal ambayo inashiriki RSL ndio imeongoza kufanya usajili wa gharama kwa kumsajili NeymaR JR kwa shilingi B 242.7 kutoka PSG.
Kwa msimu huu wa 2023/24 hivyo ndivyo vilabu vilivyofanya usajili wa pesa nyingi wakitarajia kupata matokeo mazuri kutokana na uwekezaji ambao wameufanaya. Je ni usajili upi ambao mpaka kufikia mwisho wa msimu utalipa?