Klabu ya Manchester United imeambiwa itawagharimu pauni milioni 81.5 kumsajili Jadon Sancho kutoka Borussia Dortmund baada ya kurejesha nia yao ya kumsajili mshambuliaji huyo.

United iliwabidi wasubiri miezi 12 kwa winga huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21 ili kuokoa pauni milioni 26.5 baada ya klabu hiyo ya Bundesliga kukubali kupunguza thamini ya mwaka jana ya pauni milioni 108 kwa mchezaji huyo.

Ikiwa uhamisho wa Sancho utatimia itakuwa ni rekodi ya klabu huko Old Trafford, ikiishinda Pauni milioni 80 ambazo United iliipa Leicester kwa Harry Maguire miaka miwili iliyopita.

Maslahi binafsi tayari yamekubaliwakati ya Sancho na klabu, Lakini Dortmund wanataka ada ya uhamisho ilipwe yote wakati United ingependelea kuigawanya kwa awamu.

Licha ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa tena, Dortmund bado lazima isake pesa kutoka kwa mmoja wa wachezaji wao wakubwa ili kumaliza matatizo makubwa ya kifedha ambayo wamepata wakati wa janga la coronavirus.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa