Kikosi cha Simba SC kitaingia kambini baada ya mazoezi ya leo jioni tayari kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Mchezo huo utapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili saa 10 jioni ambapo tiketi zinaendelea kuuzwa kupitia mitandao ya simu ambapo viingilio vimeshatangazwa.
Baada ya kikosi cha Simba SC kurejea kutoka nchini Botswana kilipopata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza, wachezaji walipewa mapumziko mafupi kabla ya kurejea mazoezini.
Chris Mugalu na kiungo Pape Sakho hawatakuwa sehemu ya kikosi kitachoingia kambini kutokana na kuendelea kuuguza majeraha.
Simba SC inahitaji ushindi au sare aina yoyote ili kusonga mbele katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Mchezo wa Big Bad Wolf ni moja ya michezo pendwa katika kasino zetu za meridianbet. Ukiachana na tabasamu utakalolipata wakati wa kucheza pia unajiwekea nafasi ya kuwa mshindi wa mkwanja mrefu unaotoka kila baada ya mzunguko kukamilika.


