Mahakama nchini Afrika Kusini imemhukumu kocha wa zamani wa Yanga ambaye kwasasa anaifundisha timu ya taifa ya Uganda, Milutin “Micho” Sredojevic kifungo cha miaka mitatu baada ya kukutwa na makosa mawili ya unyanyasaji wa kijinsia.

Micho aliripotiwa kufanya kosa hilo mwaka jana wakati alipokuwa akinoa Zambia. Tukio hilo lilitokea Disemba 2020 katika michuano iliyofanyika katika mji wa Port Elizabeth.
Micho alishutumiwa na mwanamke mmoja mwenye miaka 39 kushika makalio yake na kutoa kauli za udhalilishaji dhidi ya mwanamke huyo.
Mwanamke huyo alikua akifanya kazi ya kugawa kahawa uwanjani hapo, ndipo alipomuuliza kocha huyo kama atahitaji sukari kwenye kahawa yake, ambapo Mserbia huyo alisema “hapana na kisha kuongeza kwamba anataka sukarí ya aina nyingine, akionyesha kidole kwenye sehemu za siri za mwanamke huyo,” ilibainisha taarifa hiyo.
Kocha huyo amepewa ruksa ya kukata rufaa kwa mahakama za juu zaidi katika shitaka hilo linalomkabili.
Mchezo wa Big Bad Wolf ni moja ya michezo pendwa katika kasino zetu za meridianbet. Ukiachana na tabasamu utakalolipata wakati wa kucheza pia unajiwekea nafasi ya kuwa mshindi wa mkwanja mrefu unaotoka kila baada ya mzunguko kukamilika.


