Cedric Kaze kocha msaidizi wa Yanga SC ametoa ufafanuzi kwa nini klabu yake ilicheza taratibu kipindi cha pili tofauti na mwanzo katika mchezo wa jana Jumanne dhidi ya klabu ya KMC.
“ tuna safari ndefu ya kuutafuta ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara na michuano mingine ya ndani. Tulikuwa na game plan ya kucheza kwa kasi katika approach yetu ya kushambulia tukapata goli mbili . Approach ya pili ilikuwa kutunza ushindi, energy ya wachezaji pia kutafuta magoli kwa mchezo mzuri usio na purukushani kuepuka majeruhi na fatigue. Benchi la ufundi linaweka mkazo wa kila mchezo kuwa na uwezo wa kumiliki mpira , kujua majukumu yake na ya mwenzake uwanjani ili kuwa na balance nzuri kimbinu na kiufundi “ – alisisitiza Kaze akifanya mahojiano na waandishi wa habari baada ya mchezo.

Wachambuzi wengi wa soka nchini na wadau mbalimbali wa soka, wamekuwa wakiifanyia tathimini klabu ya Yanga kuwa inakata pumzi hususani kipindi cha pili. Kaze amesisitiza ni game plan yao na hubadilika kulingana na mazingira.
“ pale Kagera tulicheza soka la kasi dakika zote 90 kwakuwa tulikuwa na mpinzani ambaye mida wote alikuwa akiuweka mpira mbele ya mstari . KMC waliiga mchezo wetu wakatupa uhuru wa ku relax hivyo hakukuwa na sababu ya kuwachosha wachezaji au kucheza kwa risk.” Alisisitiza Kaze.
Cedric Kaze aliendelea kwa kusema raha ya soka ni magoli na mchezo mzuri wenye pasi nyingi ili wapenzi wa soka na wanachama wapate burudani ya timu yao .
Mchezo wa Big Bad Wolf ni moja ya michezo pendwa katika kasino zetu za meridianbet. Ukiachana na tabasamu utakalolipata wakati wa kucheza pia unajiwekea nafasi ya kuwa mshindi wa mkwanja mrefu unaotoka kila baada ya mzunguko kukamilika.


