Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Kibu Denis amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Mei (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).
Kibu ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwapiku viungo Rally Bwalya pamoja na Mzamiru Yassin.
Katika mwezi Mei, Kibu amecheza mechi saba sawa na dakika 630 akifunga mabao matano na kusaidia kupatikana kwa bao moja.
Kwa kushinda kinyang’anyiro hicho Kibu atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.
Mchanganuo wa Kura zilizopigwa na mashabiki wa Simba SC:
1. Kibu Kura 474 sawa na 84%
2. Bwalya Kura 67 sawa na 11%
3. Mzamiru Kura 19 sawa na 3%
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!