Klabu ya Simba SC imeendeleza ubabe katika uwanja wa Mkapa baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Red Arrows katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika hapo jana.

Matokeo hayo yameipa Simba SC mtaji mzuri wa mabao ambayo yatakuwa msaada mkubwa kwenye mchezo wa marudiano utakaofanyika Desemba 5 nchini Zambia.
Katika mchezo huo, Bernard Morrison alifunga bao la kwanza dakika ya 17 kwa mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja wavuni nje kidogo ya 18. Medie Kagere aliandika bao la pili dakika tatu baadaye baada ya Morrison kuwapiga chenga walinzi wa Red Arrows.
Dakika ya 31 Morrison alikosa mkwaju wa penati uliopanguliwa na mlinda mlango wa Red Arrows baada ya Hassan Dilunga kufanyiwa madhambi ndani ya 18.
Dakika ya 77 Morrison alifunga goli la tatu baada ya kuwapiga chenga walinzi wa Red Arrows na kupiga shuti la chini chini ambalo lilimshinda mlinda mlango.
Kocha wa Simba SC, Pablo Franco aliwatoa Pascal Wawa, Sadio Kanoute, Dilunga, Kagere na Rally Bwalya na kuwaingiza Henock Inonga, Mzamiru, Ibrahim Ajibu, John Bocco na Peter Banda.
Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.


