Klabu ya Simba SC imetua salama mkoani Tabora tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC utakaopigwa Ijumaa katika Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi.
Mara ya mwisho Simba SC kucheza mechi mkoani Tabora ilikuwa Aprili 18, mwaka 2017 dhidi ya Rhino Rangers ambapo ulikuwa ni mchezo wa kirafiki na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Afya za wachezaji waliokuwa wanaumwa zinaendelea kuimarika kwa kiasi kikubwa na wamesafiri na karibu kikosi kizima kwa ajili ya kutafuta alama tatu muhimu.
Taarifa zinasema Baada ya kikosi cha Simba kuwasili wachezaji watapumzika kidogo na jioni watafanya mazoezi ya kuweka miili sawa kuelekea mchezo huo.
Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.