Klabu ya Simba imeshusha viingilio kuelekea mchezo wake wa pili wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika amba unatarajiwa kupigwa siku ya jumamosi dhidi ya Raja Casablanca katika dimba la Benjamin Mkapa.
Klabu ya Simba tayari imeshapoteza mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Afrika wakiwa ugenini dhidi ya klabu Horoya, Hivo wanahitaji kushinda mchezo wao wa jumamosi dhidi ya Raja Casablanca kutoka nchini Morocco na ndio sababu ya kushusha viingilio.
Wekundu wa Msimbazi kupitia Rais wa heshima wa klabu hiyo Mo Dewji ambae ndio ameruhusu viingilio vya mchezo huo vishuke kuelekea mchezo huo wa jumamosi, Huku leongo kubwa ni kuhakikisha mashabiki wanahamasika kufika uwanjani kuipa sapoti klabu hiyo kama ambavyo imekua katika misimu iliyopita.
Klabu ya Simba imeshusha tiketi ambapo tiketi za mzunguko kutoka 5000 mpaka 3000 na VIP C kutoka 15000 mpaka 10000 VIP B kutoka 30000 mpaka 20000 na VIP A kutoka 50000 mpaka 30000 huku tiketi za Platnum na Platnum Plus tiketi zimebaki na bei yake ya kawaida.
Klabu ya Simba imekua ikitumia mashabiki kama silaha yao kubwa katika dimba lao la nyumbani Benjamin Mkapa mbali na ubora wao mkubwa ambao wamekua nao kwenye kikosi cha kwa misimu kadhaa, Hivo lengo kubwa la kupunguza viingilio ni kujaza mashabiki uwanjani ambao wamekua wakisaidia kulet ari na hamasa kwa wachezaji wa klabu hiyo na kufanikiwa kushinda mchezo.

