Trippier:Rice ni Bora Kuliko Casemiro

Beki wa kulia wa kimataifa wa Uingereza anayekipa kwenye klabu ya Newcastle Kieran Trippier amesema kua kiungo wa klabu ya West Ham Declan Rice ni bora kuliko kiungo wa Manchester United Carlos Casemiro.

Kiungo Declan Rice amekua kwenye kiwango bora kwa miaka takribani mitatu sasa ndani ya klabu ya West kitu kilichofanya Trippier aamini kua kiungo huyo ni bora zaidi ya viungo kama Carlos Casemiro pamoja kiungo wa Arsenal Thomas Partey.trippierDeclan Rice ambaye siku kadhaa nyuma kocha wake David Moyes alizungumza kua huenda ukaenda kua usajili ambao utavunja rekodi ndani ya Uingereza kama ataondoka ndani ya klabu ya West Ham, Na hiyo inatoka na kiwango ambacho anaonesha kiungo huyo.

Beki Trippier ambaye alifanya mazungumzo na na beki wa zamani wa klabu ya Manchester United Rio Ferdinand alisema kua hataki kuwakosea heshima Casemiro na Partey, Lakini anaamini kwasasa Declan Rice ni bora zaidi kutokana na namna anavyocheza na anavyotembea na mpira ni maajabu.trippierKiungo Declan Rice amekua akihusishwa kuondoka ndani ya klabu ya West Ham na mkataba wake upo mwishoni na vilabu kama Manchester United, Arsenal, na Newcastle vinatajwa sana kuwania saini ya kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.