Lebron James Bingwa Kabisa NBA

Staa wa mchezo wa kikapu kutoka nchini Marekani Lebron James amefanikiwa kuweka rekodi ya kua mfuingaji bora wa muda wote kwenye ligi kuu ya kikapu Marekani maarufu kama NBA.

Lebron James amefanikiwa kuipiku rekodi ya Kareem Al Jabbar ambae alikua mfungaji bora wa muda wote kwenye ligi kuu ya kikapu nchini marekani NBA, Lakini nyota huyo amefanikiwa kuivunja rekodi hiyo na kua kinara wa ufungaji katika ligi hiyo.Lebron jamesStaa huyo aliweza kuvunja rekodi hiyo usiku wa jana timu yake ya Los Angels Lakers ilipokua inakipiga na timu ya Oklahoma City Thunder na kufanikiwa kufunga alama 36, Hivo kumfanya kufikisha alama 38,390 huku akimpita Kareem Al Jabar aliyekua na alama 38,387.

Baada ya Lebron James kuvunja rekodi hiyo ilimfanya gwiji aliyekua anashikilia rekodi hiyo Kareem Al Jabaar aliingia uwanjani na kumpongeza staa huyo baada ya kuvunja rekodi hiyo na kufanikiwa kuweka rekodi yake mpya ndani ya ligi hiyo.Lebron jamesLebron James amefanikiwa kufikisha alama 38,390 na kua mfungaji bora wa muda wote wa ligi ya kikapu nchini marekani NBA baada ya kucheza kwa misimu 20 ya katika ligi hiyo. Pia Lebron James alionesha furaha yake baada ya kufanikiwa kuweka rekodi hiyo.

Acha ujumbe