Kocha mkuu wa klabu ya Chelsea Thomas Tuchel ameshawasili jijini Abu Dhabi kwa ajiri ya mchezo wa fainali ya Club World Cup final siku ya Jumamosi
Tuchel alikutwa na maambukizi ya Uviko-19, na kumfanya akose mchezo wa FA Cup ambao waliibuka na ushindi dhidi ya Plymouth, pia alikosa michezo mingine ya Club World Cup, na sasa anatarajia kukaa tena kwenye benchi la timu hiyo kwenye mchezo wa fainali baada ya kupimwa na kukuta hana tena maambukizi.

Chelsea waliweza kushinda michezo yao ya Club World Cup pasipo kocha tuchel, huku masidizi wake Zsolt Low akiingoza timu hiyo kwenye mchezo walioshinda dhidi ya Al Hilal kwa goli 1-0 lililofungwa na lukaku, low kwenye bench lake alikuwa akisaidiwa na mkurugenzi wa michezo Petr Cech na kocha Arno Michels.
Thomas Tuchel na klabu ya Chelsea hawajawai kuchukua ubingwa wa Club World Cup, ila Chelsea ilifanikiwa kucheza fainali mwaka 2012 na kufungwa na timu kutoka Brazili Corinthians jijini Yokohama, na Jumamosi hii tena wanakutana na timu kutoka Brazili Palmeiras.
Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.


